1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Marekani na UK zaendeleza mashambulizi dhidi ya wahouthi

23 Januari 2024

Marekani na Uingereza wameendeleza mashambulizi yao ya pamoja ya kijeshi kwa siku ya pili leo dhidi ya waasi wa Houthi kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na waasi hao katika Bahari ya Shamu.

https://p.dw.com/p/4ba6t
Yemen | Mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za Wahouthi Yemen
Mashambulizi ya vikosi vya Marekani na washirika wake vimelenga maeneo 8 ya Wahouthi nchini Yemen.Picha: CENTCOM/Anadolu/picture alliance

Marekani na Uingereza wameendeleza mashambulizi yao ya pamoja ya kijeshi kwa siku ya pili leo dhidi ya waasi wa Houthi kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na waasi hao katika Bahari ya Shamu. Waasi hao wanaoungwa mkono na Iran wameapa kulipiza kisasi.

Mashambulizi ya leo yaliyofanyika mapema alfajiri yaliyosikika mjini sanaa nchini Yemen, yanadaiwa kulenga maeneo nane ya wahouthi.

Soma pia: Marekani na Uingereza zafanya duru mpya ya mashambulizi dhidi ya waasi wa Kihuothi

Uingereza na Marekani waliwashambulia kwa mara ya kwanza waasi hao mapema mwezi huu na Marekani ikaanzisha shambulizi jengine la angani dhidi ya makombora ya wahouthi iliyosema inatoa kitisho kwa raia na meli za kijeshi. 

Hata hivyo, waasi hao wameapa kuendelea kushambulia ikiwa ni sehemu moja ya mzozo unaokuwa Mashariki ya Kati unaofungamanishwa na vita vya Israel na Hamas uliozua wasiwasi wa kutanuka kwa vita vitakavyoihusisha Iran.