1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Israeli zataka mazungumzo mengine kati ya rais wa Palestina na chama cha Hamas

19 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAw

Marekani na Israeli zimemtaka rais wa Palestina Mahmud Abbas kutosimamisha kabisa mazungumzo yake na serikali yenye kuongozwa na chama cha Hamas ambayo ilikataa kusimamisha machafuko na kukubali taifa la Israeli. Waziri wa Marekani wa mambo ya kigeni bibi Condoleeza Rice na mwenzake wa Israeli Tzipi Livni wamemuambia rais Abbas mjini New York kwamba hakutakuwepo na maridhiano yoyote yale juu ya masharti yaliyowekwa na jumuiya ya kimataifa. Rais wa Palestina Mahmud Abbas, anatarajiwa kuanza tena majadiliano na chama chenye msimamo mkali cha Hamas mara tu baada ya kurudi nyumbani kutoka New York kwenye mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa mataifa. Majadiliano hayo na kundi la Hamas, yamependekezwa baada ya rais Abbas kuwa na mazungumzo na rais wa Marekani George W. Bush. Mkutano huo kati ya viongozi hao wawili, ulikuwa ni wa kwanza tangu mwezi Oktoba mwaja jana. Wakati huo huo, nchi za Kiarabu zinatafuta mbinu nyingine ya kuanzisha mazungumzo ya amani katika eneo la mashariki ya kati.