1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani, Japan na India zatangaza mikakati ya kiusalama

29 Julai 2024

Wanadiplomasia wa ngazi za juu kutoka Japan, Marekani, Australia na India wanaokutana leo mjini Tokyo wameorodhesha hatua za kuchukua katika kulinda usalama wa safari za baharini.

https://p.dw.com/p/4ir6E
Japan - Marekani Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, katikati, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Yoko Kamikawa wakati wa mkutano mjini Tokyo, Jumapili, Julai 28, 2024. Picha: Hiro Komae/AP/picture alliance

Wanadiplomasia hao wamejadili pia njia za kusimamia usalama wa kimtandao na kuzisaidia nchi nyingine za Asia na Pasifiki katika kuimarisha mifumo yao ya ulinzi.

Hatua hiyo inachukuliwa kufuatia kuongezeka kwa mivutano katika maeneo ya  bahari ya kanda hiyo.

Soma pia: NATO yalenga kukabiliana na ushawishi wa China 

Mawaziri wa mambo ya nje wa Japan, Marekani Australia na India wamesema wana wasiwasi mkubwa kuhusu mivutano iliyopo na wamekosoa vikali hatua zinazochukuliwa na China katika eneo la bahari ya Kusini mwa China.

Serikali nyingi za kanda hiyo zinapingana na madai ya China kuhusu kumiliki eneo bahari ya Kusini mwa China ambalo ni eneo muhimu kwa shughuli za kibiashara na kuna uwezekano wa kuwepo nishati katika eneo hilo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW