1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Marekani na Iran kubadilishana wafungwa

18 Septemba 2023

Tehran imesema zoezi hilo litafanikiwa ikiwa watapokea fedha zao zipatazo bilioni 6 zilizokuwa zimezuiliwa na mshirika wa Marekani, Korea Kusini, kufuatia vikwazo vya kimataifa.

https://p.dw.com/p/4WSdr

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema itabadilishana wafungwa na Marekani baadaye leo. Tehran imesema zoezi hilo litafanikiwa ikiwa watapokea fedha zao zipatazo dola bilioni 6 zilizokuwa zimezuiliwa na mshirika wa Marekani, Korea Kusini, kufuatia vikwazo vya kimataifa.

Kwa  mujibu wa makubaliano hayo, fedha hizo zinahamishwa kutoka Korea Kusini hadi Qatar na kisha  Tehran itawaachilia raia watano wa Marekani huku Washington ikiwaachilia Wairani watano.

Rais wa Iran Ebrahim Rais anatarajiwa pia kutoa hotuba katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, zoezi hilo la kubadilishana wafungwa halimaanishi kuwa mvutano kati ya Marekani na Iran umepunguwa. Bado Marekani inaituhumu Iran kuwa inaendelea kurutubisha urani kwa viwango vya juu katika mpango wake wa kumiliki silaha za nyuklia.