1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yazuka upya kati ya M23 na vijana wazalendo Kongo

19 Juni 2023

Mashirikia ya kiraia katika wilaya ya Masisi huko mkoani Kivu kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yametangaza kuzuka upya kwa mapigano kati ya waasi wa M23 na makundi ya vijana wanaojiita wazalendo.

https://p.dw.com/p/4SlVo
Konflikt im Kongo | M23 Soldaten
Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Hali iliendelea kuwa ya wasiwasi mchana kutwa wa Jumamosi kuamkia jana Jumapili kwenye vijiji vya Kahira, Kasopo na Buhimba eneo la Bashali katika wilaya ya masisi ,ambako waasi wa M23 wilizishambulia ngome za vijana hao wazalendo. Hadi sasa mamia ya raia wameendelea kukimbia na kueleka katika vijiji jirani vya lushebere, mweso na Kahanga huku waasi wa M23 wakijiimarisha kwenye milima inayoinukia maeneo yanayokaliwa na vijana hao wanaojiita wazalendo na kuifanya hali ya kiutu kuwa mbaya zaidi, alielezea telesphore MITONDEKE mratibu wa asasi za kiraia wilayani Masisi.

Kongo I Treffen zwischen EACRF und  M23-Rebellen
Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki lipo KongoPicha: Guerchom Ndebo/AFP

Soma pia:Waasi wa M23 wahusishwa na makaburi ya pamoja nchini DRC

Hata hivyo, hali ya taharuki imekuwa ikishuhudiwa tangu Jumatano baada ya kuonekana kwa misururu ya waasi wa M23 katika vijiji hivyo vyenye utajri wa kilimo. Akizungumza na DW, Heritier NDANGENDANGE msemaji wa vijana hao wazalendo amedai kuwa wamefaulu kuyadhibiti  upya maeneo walikotimuliwa baada ya mapigano makali yaliyodumu kwa saa kadhaa.

Vurugu katika eneo hilo zimeendelea licha ya wito wa hivi karibuni wa viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki kulitaka kundi hilo kuondoka na kusitisha mapigano, hali ambayo imesalia kuwa kitendawili. Etienne KAMBALE ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika ukanda huu.

Haya yanajiri wakati huu ampapo, kundi la wataalamu wa umoja wa mataifa kuhusu Congo, lilisema hiyo jana Jumapili kukaribia kuchapisha ripoti ambayo inathibitisha kwamba jeshi la Rwanda linaendelea kuhakikisha uwepo katika ardhi ya Congo ili kuwaunga mkono waasi wa M23, lawama ambazo zinaonekana kutopunguza kasi ya kigali ambayo bado inakanusha kuhusika kwa vyovyote vile.