1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Mapigano yaua watu 74 nchini Somalia

10 Februari 2023

Idadi ya vifo kutokana na mapigano katika eneo lenye mamlaka ya ndani Somaliland Somalia imeongezeka na kufikia watu 74.

https://p.dw.com/p/4NL86
Somalia Höhlen von Laas Geel
Picha: Imago/robertharding/M. Runkel

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa mji unaokabiliwa na mapigano wa Las Anod.

Ghasia zilizuka katika mji huo siku ya Jumatatu, muda mfupi baada ya majimbo matatu katika eneo lililojitenga la Somaliland katika Pembe ya Afrika kutangaza kutaka kuwa sehemu ya Somalia tena.

Majimbo ya Sool, Sanaag na Cayn yanaunda takriban theluthi moja ya majimbo ya mamlaka ya Somaliland.Maeneo hayo yanazozaniwa pande zote mbili Somaliland na mamlaka ya jirani ya Puntland.

Vurugu katika ukanda huo zimedumu kwa majuma kadhaa sasa.