Mapigano Mashariki mwa Kongo yazuka upya
16 Septemba 2008Matangazo
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yuko katika ziara ya eneo hilo la mapigano la Kivu ya Kaskazini na inaelezwa hadi sasa hakutoa taarifa yoyote ile hadharani juu ya ziara yake hiyo ambayo ni nadra kufanya katika eneo la mapigano.
Mohamed Dahman alipata fursa ya kuzungumza na mkaazi mmoja wa Goma mji mkuu wa Kivu ya Kaskazini Paterne Inga juu ya mapigano hayo.