Mapigano mapya yatokea Cote d'Ivoire
24 Februari 2011Matangazo
Siku moja kabla, wafuasi hao wa Ouatarra walifanikiwa kuwafurusha wanajeshi wa hasimu wake. Ghasia hizo zinatokea wakati ambapo juhudi za kuutanzua mzozo huo kidiplomasia zinaendelea. Mapema wiki hii jopo maalum la marais liliizuru Abidjan na wakakutana na washirika wakuu wa kisiasa wa Cote d'Ivoire. Mzozo huo wa kisiasa umesababishwa na mvutano kati ya Alassane Ouatarra na mpinzani wake mkuu Laurent Gbagbo wanaodai kuwa washindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Novemba mwaka uliopita.