1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano makali yaendelea mjini Khartoum, Sudan

4 Mei 2023

Mapigano makali yameshuhudiwa mapema leo katikati ya mji wa Khartoum nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4Qssr
Mapigano nchini Sudan
Mapigano yamesababisha uharibifu nchini Sudan Picha: picture alliance / AA

Jeshi la nchi hiyo limekuwa likijaribu kukisukuma nyuma kikosi chenye nguvu cha wanamgambo wa Rapid Support (RSF), kutoka viunga vya ikulu ya rais na karibu na makao makuu ya jeshi.

Umoja wa Mataifa unawashinikiza majenerali wanaohasimiana Sudan wahakikishe usalama kwa misafara ya magari ya misaada ya kiutu baada ya malori sita ya misaada kuporwa. 

Mapigano hayo yakiendelea, usitishaji mapigano wa kudumu unaonekana kutowezekana.

Kila upande unaonekana kupigania udhibiti wa mji mkuu kuelekea uwezekano wa kufanyika mazungumzo ya amani.