1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

vita Khartoum kitisho kwa mpango wa kusitishwa mapigano

20 Aprili 2023

Wanajeshi kutoka pande mbili hasimu nchini Sudan wamekabiliana leo karibu na kambi kuu ya kijeshi katikati ya Khartoum na maeneo mengine ya mji mkuu leo.

https://p.dw.com/p/4QMlJ
Sudan Khartum | Flucht Bewohner vor Kämpfen
Picha: AFP

Makabiliano hayo yanatishia kuvuruga juhudi za karibuni za mpango wa kusitishwa mapigano wakati serikali za kigeni zikitafuta mbinu za kuwahamisha raia wao waliokwama katika mzozo huo.

Mpango wa kuweka chini silaha kwa saa 24, ambao ulianza kutekelezwa jana jioni, ndio jaribio kubwa kabisa mpaka sasa la kusitisha mapigano hayo kati ya jeshi na vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces - RSF. Kiasi ya watu 330 wameuawa na 3,300 kujeruhiwa katika mapigano hayo tangu yalipoanza Jumamosi, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani - WHO lakini idadi huenda ikawa kubwa kwa sababu miili zaidi inapatikana mitaani. Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kujaribu kuyarefusha makubaliano ya kusitishwa mapigano.