Kashfa ya kampuni ya Volkswagen
22 Septemba 2015Wahariri hao pia wanauzungumzia ushindi wa chama cha Syriza katika uchaguzi wa bunge nchini Ugiriki.
Gazeti la "Badische Neueste Nachrichrichten" linasema kampuni ya magari ya Ujerumani ya Volkswagen.imejiharibia sifa .Kampuni hiyo iliunda kifaa cha kuonyesha viwango vya kuchafuka k wa mazingira. Lakini kifaa hicho kimegundulika kuwa bandia. Kimekuwa kinatoa vipimo vya uwongo juu ya kuchafuka kwa mazingira.
Mhariri wa gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" anasema licha ya hasara kubwa ya fedha ambayo hadi jana ilifikia karibu Euro Bilioni 17,iliyosababishwa na kashfa hiyo, kampuni ya Volkswagen imejiharibia sifa kwa kiwango kikubwa.
Mhariri wa gazeti la "Thüringische Landeszeitung" anataka hatua zichukuliwe kwa wanaohusika na kashfa hiyo. Mhariri huyo anasema kampuni ya magari ya Volkswagen liekeza fedha katika kutengeneza kifaa cha kuinufaisha kampuni hiyo badala ya kulinda mazingira.
Inavyoekelea inapohusu mambo ya ubunifu kampuni hiyo inayo watu hodari. Lakini ikiwa itathibitishwa kwamba hadaa hiyo ilifanyika kwa makusudi, viongozi wote wa kampuni hiyo watapaswa wajiuzulu.
Na mhariri wa gazeti la "Donaukurier" anasema ni vigumu kuamini kwamba udanganyifu huo ulifanyika bila ya viongozi wa kampuni kuwa na habari. Mhariri huyo pia anasema viongozi wa Volkswagen watapaswa wajiuzulu, ikiwa itathibika kwamba walijua juu ya udanganyifu uliofanyika.
Gazeti la "Thüringer Allgemeine" linatoa maoni juu ya ushindi wa Mwenyekiti wa chama cha Syriza, Alexis Tsipras, katika uchaguzi wa Bunge nchini Ugiriki.
Mhariri wa gazeti hilo anasema kwamba Alexis Tsipras hatakuwa na uwanja mkubwa . Kwa mujibu wa makubaliano aliyofikia na Umoja wa Ulaya, Tsipras atakuwa na kiasi kidogo cha fedha, lakini anatakiwa aendelee kubana matumizi.
Lakini linahoji kwamba masharti hayo pia yanatoa fursa. Ikiwa atathibitisha kwamba anayaleta mageuzi kwa moyo wote, huenda suala la Ugiriki kupunguziwa madeni likajadiliwa na Umoja wa Ulaya. Lakini kwanza lazima Tsipras ajenge imani miongoni mwa wakopeshaji wake.
Gazeti la "Badische" linasema Papa Francis amewavunja moyo wapinzani kisiwani Cuba. Mhariri huyo anasema wapinzani wengi wamevunjwa moyo na ziara ya Baba Mtakatifu kwa sababu walitumai kuwa hali yao ingekuwa nzuri laiti Papa Francis angeliweka mkazo juu ya suala la haki za binadamu.
Mwandishi: Mtullya abdu/Deutsche Zeitungen/
Mhariri: Mohammed Khelef