1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mamluki wa Wagner wakiri wapiganaji wake wameuwawa

29 Julai 2024

Kundi la wapiganaji mamluki kutoka Urusi la Wagner limesema wapiganaji wake pamoja na wanajeshi wa Mali wameuliwa katika mapigano makali dhidi ya waasi wa Tuareg karibu na mpaka wa Mali na Algeria.

https://p.dw.com/p/4irKS
Mali Kidal | Uratibu wa Harakati za Azawad CMA
Wapiganaji wa kundi la Uratibu wa Harakati za Azawad (CMA) wakishika doria wakati wa Kongamano la kujadili ushirikiano na makundi yenye malengo sawa mjini Kidal.Picha: SOULEYMANE AG ANARA/AFP/Getty Images

Katika hatua isiyo ya kawaida, kundi hilo limetoa taarifa likisema wanajeshi wake waliokuwa wakipambana bega kwa bega na wanajeshi wa Mali kuanzia Julai 22 hadi 27 walizidiwa nguvu kwenye mapambano yaliyokuwa yakiongozwa na kamanda Sergei Shevchenko karibu na mji wa Tinzaouaten.

Soma pia: Uingereza inapanga kulipiga marufuku kundi la Wagner 

Katika ujumbe uliochapishwa na katika ukurasa wa Telegram, Wagner imesema ilifanikiwa kuwaangamiza wapiganaji wengi wa itikadi kali.

Hata hivyo kimbunga cha mchanga kilichopiga kwenye eneo hilo kiliyasaidia makundi hayo kujipanga upya na kuwazidi nguvu wapiganaji wa Wagner na wanajeshi wa Mali.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW