1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiKorea Kusini

Mamia wahamishwa kutokana na moto mkubwa Korea Kusini

11 Aprili 2023

Mamia ya raia nchini Korea Kusini wamelazimika kukimbia makaazi yao baada ya moto wa nyikani kusambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali na kuharibu nyumba kadhaa katika mji wa pwani wa Gangneung.

https://p.dw.com/p/4Pu2B
Südkorea | Waldbrand nahe der Stadt Samcheok
Picha: Yonhap/picture alliance

Wafanyakazi karibu 3,000 wa zimamoto walitumia masaa yapatayo manane kujaribu kuuzima moto huo ulioanzia kwenye mlima uliopo katikati ya mji huo, majira ya saa 2.30 usiku.

Karibu nyumba 70 na majengo mengine yaliungua na zaidi ya watu 550 waliondolewa na kupelekwa kwenye maeneo salama.

Hata hivyo,  hakukua na ripoti yoyote ya kifo kilichosababishwa na moto huo,   ambao pia ulipunguzwa kasi na mvua, ingawa baadhi ya raia na wazima moto waliripotiwa kupata majeraha makubwa ya moto.