Malori ya misaada yaanza kuingia Gaza
19 Januari 2025Kupitia mtandao wa kijamii wa X, afisa mkuu wa muda wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada la OCHA kwa maeneo ya Palestina, Jonathan Whittall, amesema lori la kwanza la misaada ya kiutu limeingia katika Ukanda wa Gaza mara baada ya makubaliano kuanza kutekelezwa.
Soma pia: Usitishaji mapigano waanza kutekelezwa Gaza
Huku haya yakijiri Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ilikuwa muhimu kwa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza kati ya Israel na Hamas hatimaye kutekelezwa na hatimaye mateka waliobaki kuachiliwa.
Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis ametoa shukrani kufuatia usitishwaji vita Gaza na kusifu dhima ya wapatanishi waliohusika.
Soma pia: Israel itawaachilia zaidi ya wafungwa 1900 wa Kipalestina
Papa Francis aliwashukuru wote waliohusika katika kufanikisha mpango huo, akiwaombea mateka wote waweze kurudi nyumbani na kuwakumbatia tena wapendwa wao.