1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yaanzisha uchunguzi dhidi ya washukiwa wa ugaidi

29 Novemba 2023

Mahakama nchini Mali imetangaza kuanzisha uchunguzi dhidi ya viongozi kadhaa wanaopigania kujitenga na walio na mahusiano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda kuhusu tuhuma za ugaidi na utakatishaji fedha.

https://p.dw.com/p/4ZZbJ
Waasi wa Tuareg
Waasi wa TuaregPicha: Souleymane Ag Anara/AFP

Wanaochunguzwa ni pamoja na Iyag Ag Ghaly, kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Tuareg na kiongozi wa muungano wa Kiislamu na Waislamu unaohusishwa na kundi la al-Qaeda, na mhubiri wa msimamo mkali kutoka kabila la Fulani Amadou Koufa, ambaye ni mwanachama wa kundi hilo.

Pia kwenye orodha hiyo, ni viongozi sita wa Tuareg wanachama wa muungano wa makundi ya wapiganaji ambao hivi karibuni ulianzisha upya uasi dhidi ya taifa, licha ya kusaini muafaka wa amani mwaka wa 2015 mjini Algiers.

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali imesema uchunguzi huo ulianzishwa sio tu dhidi ya viongozi wa kigaidi bali pia wanachama waliosaini makubaliano ya amani ya mwaka wa 2015 na wamejiunga na ugaidi.