1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makumbusho ya wahanga wa maovu ya wanazi yafunguliwa mjini Berlin

11 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEe

Berlin:

Israel imesifu makumbusho ya mauwaji ya kikatili yaliyofanywa na wanazi katika vita vikuu vya pili vya dunia.Taarifa rasmi ya serikali imeitaja serikali kuu ya Ujerumani kua ni „mshirika katika kupambana na hisia za chuki dhidi ya wayahudi.“Masaa kadhaa kabla ya hapo makumbusho hayo ya mauwaji ya wayahudi barani Ulaya yalifunguliwa katika uwanja mkubwa nyuma ya lango la Brandenburger Tor mjini Berlin.Mchora ramani maarufu wa kimarekani Peter Eisenman amesema makumbusho hayo yanachukua nafasi ya kauli kwa Ujerumani na ulimwengu mzima.Spika wa bunge la shirikisho Bundestag Wolfgang Thierse amesisitiza,makumbusho hayo,hayamaanishi yaliyofanywa na wanazi ndo yatasahauliwa.Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya wayahudi Paul Spiegel,mbali na kusifu makumbusho hayo,amelalamika pia akisema makumbusho hayo hayawadhukuru waliofanya maovu.