1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makamu wa zamani wa rais wa Equador alazwa hospitalini

9 Aprili 2024

Makamu wa zamani wa rais wa Equador, Jorge Glas, anaripotiwa kulazwa hospitalini baada ya kugoma kula, kwa mujibu wa mamlaka ya magereza nchini humo.

https://p.dw.com/p/4eYxV
Ecuador  Jorge Glas
Makamu wa zamani wa rais wa Equador, Jorge Glas.Picha: Photoshot/picture alliance

Glas, mwenye umri wa miaka 54, aliripotiwa kuwako kwenye hospitali ya jeshi la majini mjini Guayaquil, alikokuwa anaendelea na matibabu.

Vyombo vya usalama vya Equador viliuvamia ubalozi wa Mexico siku ya Ijumaa na kumkamata makamu huyo wa zamani wa rais, masaa machache baada ya kupatiwa hifadhi ya kisiasa.

Uvamizi huo umesababisha mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo, huku rais wa Mexico akimlaumu mwenzake wa Equador kwa utawala wa kidikteta.

Mapema siku ya Jumatatu (Aprili 8), mwanasheria wake mjini Brussels aliliambia shirika la habari la AFP kwamba anahofia usalama wa maisha ya mteja wake na akomba msaada wa kimataifa.

Polisi iliadai kuwa Glas, anayetuhumiwa kwa ufisadi, alizimia kwa makusudi baada ya kumeza vidonge vya kukabiliana na mfadhaiko.