Miaka 30 iliyopita, makaburi ya watu wengi yaligunduliwa Belarus. Baada ya kufukuliwa ilijulikana kwamba wahanga hao wanaofika robo milioni waliuawa wakati wa takasatakasa ya kiongozi wa zamani wa Jamhuri ya Kisovieti, Joseph Stalin. Ungunduzi huo umezua maandamano. Ungana na Iddi Sessanga katika Mwanagaza wa Ulaya.