1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Kongo, Burundi zashirikiana kuwazuia M23 kuelekea Kusini

Angela Mdungu
1 Februari 2025

Wanajeshi wa Kongo wakisaidiana na jeshi la Burundi wamefanya juhudi za pamoja kuwarudisha nyuma waasi wa M23 waliokuwa wakisonga mbele mashariki mwa Kongo na kuelekea katika mji mkuu wa Kivu Kusini wa Bukavu.

https://p.dw.com/p/4pvKR
Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Waasi wa M23 wakiwa na wanajeshi na polisi wa Jamhusi ya Kidemokrasia ya Kongo waliojisalimisha GomaPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Mapema wiki hii waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda waliuteka mji mkuu wa Kivu Kaskazini wa Goma baada ya mapigano makali na wameapa kusonga mbele hadi kuelekea mji mkuu Kinshasa.

Soma zaidi:Kongo: Mji wa Bukavu wachukua tahadhari dhidi ya M23 

Hayo yanajiri muda mfupi baada ya viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kutoa tamko la dharura la kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mapambano yake dhidi ya M23 . SADC ilifanya mkutano wa dharura nchini Zimbabwe kuhusu mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo, ambao umeibua wasiwasi kuhusu usalama wa kikanda.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa, watu 700 wameshauwawa kutokana na mzozo huo katika kipindi kisichozidi wiki moja.