1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maiti nyingine 11 zafukuliwa katika msitu wa Shakahola

11 Mei 2023

Maiti nyengine kumi na moja zilifukuliwa jana katika msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya hali iliyoongeza idadi ya maiti kufikia 145.

https://p.dw.com/p/4RDQY
Kenyans seek relatives among starvation cult victims in Malindi
Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Maiti nyengine kumi na moja zilifukuliwa jana katika msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya hali iliyoongeza idadi ya maiti kufikia 145.

Kulingana na mkuu wa mkoa wa Pwani Rhoda Onyancha, watu 579 ambao wanahusishwa kujiunga na dhehebu la mhubiri Paul Mackenzie huko Kilifi hawajulikani waliko kufikia sasa, na tayari watu 14 wameunganishwa na familia zao.

Watu wengine wawili wameokolewa wakiwa hai, idadi ya waliookolewa kwa sasa ni watu 70. Shughuli ya kuifukua miili awamu ya pili imeingia siku ya tatu leo.

Kulingana na waziri wa uslama wa ndani Kithure Kindiki, tukio hilo ni moja ya janga kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Kenya.