1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoItaly

Mahasimu wa Milan kukutana nusu fainali ya Champions League

Sylvia Mwehozi
20 Aprili 2023

Inter Milan wametinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 na Benfica na sasa watavaana na AC Milan katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.

https://p.dw.com/p/4QK57
Fußball UEFA Champions League | Inter Mailand v Benfica Lissabon
Picha: HochZwei/Syndication/IMAGO

Inter Milan wametinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 na Benfica na kuwafanya Waitaliano hao kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-3. Mabao kutoka kwa Nicolo Barella, Lautaro Martinez na Joaquin Correa yalifanikiwa kuipeleka Inter hatua ya nusu fainali na itakabiliana na AC Milan.

Inter walichukua uongozi katika dakika ya 13 kwa shuti kali la Nicolo Barella kutoka ndani ya eneo la hatari lakini Benfica walisawazisha dakika ya 38 kupitia kwa Fredrik Aursnes aliyefunga kwa kichwa. Mechi za nusu fainali zitachezwa mnamo tarehe 9 mwezi ujao.