1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yawaachia wapinzani 11 Mali

6 Desemba 2024

Mahakama moja nchini Mali imewaachilia huru wapinzani 11 waliokamatwa kwa tuhuma za kula njama dhidi ya mamlaka za nchi, baada ya kutoa wito wa kurejeshwa utawala wa kiraia.

https://p.dw.com/p/4noq0
Mali, Jenerali Abdoulaye Maïga
Naibu waziri mkuu wa Mali, Jenerali Abdoulaye Maiga.Picha: Bryan R. Smith/AFP

Chanzo kimoja cha mahakama hiyo na mmoja kati ya walioachiliwa huru wamesema miongoni mwa walioachiliwa ni mawaziri wa zamani na viongozi wa vyama vya siasa na asasi za kiraia, ambao mnamo mwezi Machi walisaini tamko la kulitaka jeshi kurejesha madaraka kwa raia.

Watu hao walikamatwa mwezi Juni kwa kula njama dhidi ya mamlaka halali na kufanya mkutano haramu, wakati walipokutana kwenye nyumba ya mmoja wao mjini Bamako.

Soma zaidi: Mali yawakamata maafisa wanne waandamizi wa kampuni ya madini ya Canada

Taifa hilo la magharibi mwa Afrika limekuwa kwenye mzozo wa kisiasa na kiuchumi na pia ghasia za makundi yenye silaha tangu mwaka 2012.

Mnamo mwezi Juni 2022, utawala wa kijeshi ulitangaza kwamba ungerejesha serikali ya kiraia mwishoni mwa mwezi Machi 2024.