1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Senegal kuamua hatima ya kiongozi wa upinzani

6 Desemba 2023

Mahakama nchini Senegal itaamua endapo kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko, anapaswa kurudishwa katika daftari la uchaguzi, hatua ambayo itaamuwa kuhusu hatima yake ya kugombea uchaguzi ujao wa rais.

https://p.dw.com/p/4ZpkZ
Kiongozi wa upinzani wa Senegal, Ousmane Sonko.
Kiongozi wa upinzani wa Senegal, Ousmane Sonko.Picha: Seyllou/AFP

Kwa mujibu wa taarifa ya mahakama ya rufaa, kikao maalum cha kusikiliza kesi hiyo kimepangiwa kufanyika Desemba 12.

Kiongozi huyo wa upinzani aliondolewa kwenye daftari la uchaguzi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mnamo mwezi Juni baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na upotoshaji vijana kimaadili.

Soma zaidi: Sonko aanza tena mgomo wa kula
Kiongozi wa upinzani Senegal Sonko arejeshwa gerezani baada ya kutibiwa hospitalini

Mwanasiasa huyo amekuwa katikati ya mvutano na serikali kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili hali iliyozusha machafuko mara kadhaa nchini Senegal.

Sonko anadai kesi zinazomuandama zimetengenezwa kwa lengo  kumzuia kugombea uchaguzi wa rais,madai ambayo serikali imeyakanusha ikisema haina ushawishi katika mfumo wa mahakama.