1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUlaya

Mahakama kuu ya Ulaya yaamuru Google na Apple kulipa kodi

10 Septemba 2024

Mahakama kuu ya Umoja wa Ulaya imeyaamuru makampuni ya teknolojia ya Google na Apple kulipa mabilioni ya kodi ambayo hayakuilipa mwanzo na faini ya ushindani mtawalia.

https://p.dw.com/p/4kTWP
Logo za Google na Apple
Mahakama Kuu ya Ulaya imeyataka makampuni makubwa ya teknolojia ya Google na Apple kulipa kodi na kuhitimisha mizozo ya muda mrefu ya kisheria.Picha: Pavlo Gonchar/SOPA Images/IMAGO

Kesi hizo mbili zilikuwa sehemu ya mapambano ya Umoja wa Ulaya kukomesha mianya ya kodi na udhibiti wa makampuni makubwa ya teknolojia ya Marekani.

Mahakama ya Haki ya Ulaya ECJ imeunga mkono hukumu iliyotolewa mwaka 2016 na Tume ya Ulaya kwamba Apple inapaswa kulipa kodi ya euro bilioni 13 na kubatilisha uamuzi wa awali uliokuwa upande wa Apple.

Tume ya Ulaya ilisema katika hukumu ya mwaka 2016, kuwa kampuni ya Apple ililipa kodi kidogo kufuatia makubaliano yasiyo halali na mwanachama wa Umoja wa Ulaya Ireland.