1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mahakama kuu ya Israeli kusikiliza rufaa ya sheria mpya

26 Julai 2023

Mahakama kuu ya Israeli imesema itasikiliza rufaa dhidi ya sheria mpya inayopunguza baadhi ya mamlaka yake na kuiweka katika mkondo wa mgongano na serikali ya mrengo mkali wa kulia ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

https://p.dw.com/p/4UQcZ
Maandamano dhidi ya sheria mpya nchini Israel 24.07.2023
Maandamano dhidi ya sheria mpya nchini IsraelPicha: Oded Balilty/AP Photot/picture alliance

Mapema wiki hii serikali ya mseto iliidhinisha marekebisho yanayoiwekea mahakama mpaka wa kuweza kuyabatilisha maamuzi ya serikali na ya mawaziri itakapoyaona kuwa hayana busara. Bunge la Israel liliyapigia kura mabadiliko hayo bila ya wabunge wa upinzani ambao walisusa kupiga kura.

Mabadiliko yalitifua maandamano

Kupitishwa mabadiliko hayo kulitifua maandamano zaidi nchini Israel. Kwa mujibu wa uamuzi wa majaji uliotangazwa kwenye tovuti, kesi hiyo ya rufaa itasikilizwa mnamo mwezi wa Septemba. Mahakama ya juu ya Israel haikutoa pingamizi dhidi ya sheria mpya.