1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yabatilisha hukumu ya kifo cha rapa maarufu Iran

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Mahakama kuu ya Iran imebatilisha hukumu ya kifo dhidi ya mwanamuziki maarufu Toomaj Salehi ambaye alifungwa jela kwa kuunga mkono maandamano ya nchi nzima yaliyotokana na kifo cha msichana Mahsa Amini.

https://p.dw.com/p/4hOGN
Mwanamuziki maarufu wa Iran Toomaj Salehi
Mwanamuziki maarufu wa Iran Toomaj Salehi Picha: Le Parisien/Arnaud Journois/MAXPPP/dpa/picture alliance

Mahakama kuu ya Iran imebatilisha hukumu ya kifo dhidi ya mwanamuziki maarufu Toomaj Salehi ambaye alifungwa jela kwa kuunga mkono maandamano ya nchi nzima yaliyotokana na kifo cha msichana Mahsa Amini. Wakili wake Amir Raisian amesema kupitia ukurasa wa mtandao wa X kwamba mahakama ya juu ya Iran pia imeamuru kusikilizwa upya kwa kesi.

Mnamo mwezi Aprili, mahakama ya Iran ilimhukumu adhabu ya kifo mwanamuziki huyo kwa kosa la "ufedhuli". Rapa huyo pia alikutwa na hatia ya makosa mengine ya uchochezi, mikusanyiko na kula njama, propaganda dhidi ya serikali na kuchochea ghasia.

Salehi alikamatwa Oktoba mwaka 2022 baada ya kuunga mkono hadharani maandamano yaliyozuka mwezi mmoja kabla, yakichochewa na kifo cha Mahsa Amini.