1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Mahakama Kongo yawahukumu kifo watu 37 waliojaribu mapinduzi

14 Septemba 2024

Mahakama ya Kijeshi nchini Kongo imewahukumu adhabu ya kifo watu 37, wakiwemo Wamarekani watatu, baada ya kuwatia hatiani kwa mashtaka ya kushirki katika jaribio la mapinduzi.

https://p.dw.com/p/4kcSw
Kongo - gereza la Ndolo mjiniKinshasa
Kongo - gereza la Ndolo mjini KinshasaPicha: Arsene Mpiana/AFP

Washtakiwa hao, wengi wao wakiwa raia wa Kongo, lakini wakiwemo pia Muingereza, Mbelgiji na Mcanada, wana muda wa siku tano kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, inayohusisha pia mashtaka ya ugaidi na ushirika wa uhalifu.

Watu 14 wameachiwa huru katika kesi hiyo iliyoanza mwezi Juni. Watu sita waliuawa wakati wa jaribio hilo lililoongonzwa na mpinzani asiemaarufu Christian Malanga mnamo mwezi Mei, ambalo lililenga kasri la rais na mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi.

Malaga aliuawa katika ufyatulianaji risasi na vikosi vya usalama vilipojaribu kumkamata, na mtoto wake Marcel Malanga, ambaye ni raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 21 ni miongoni mwa waliohukumiwa kifo.