1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magufuli achukua fomu ya urais

6 Agosti 2020

Rais wa Tanzania John Magufuli amechukua fomu ya kuwania muhula wa pili wa kutoka tume ya taifa ya uchaguzi NEC, akiahidi kuendesha kampeni za kistaarabu kueleka uchaguzi hwa Oktoba.

https://p.dw.com/p/3gVn8
Tansania Dodoma | Wahlkampf | CCM Partei
Picha: DW/S. Khamis

Majira ya saa tatu na dakika arobaini kwa saa za Afrika Mashariki mgombea alieteuliwa na chama tawala CCM na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli akiwa ameambatana na mgombea mwenza ambae pia ni makamu wa rais Samia Suluhu na viongozi wengine wa chama waliwasili katika jengo jipya la tume ya taifa ya uchaguzi mjini Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu ya urais.

Akimkabidhi fomu hiyo iliolipiwa kiasi cha shilingi za Tanzania milioni moja, mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC jaji mstaafu semistokles kaijage amesema, mkoba wa fomu umesheni nyaraka kadhaa ambazo mgombea huyo atalazimika kuzijaza ikiwemo kupata wadhamini wasiopungua mia mbili kutoka mikoa 10 ikiwemo 2 ya Zanzibar huku idadi jumla ya wadhamini wanaohitajika kwa mujibu wa sheria ikiwa ni 2000.

Punde baada ya kumaliza zoezi hilo la kisheria na kidemokrasia mgombea huyo alianza safari ya kuelekea katika ofisi za makao makuu ya chama chake.

Rais Magufuli asema anawania muhula wa pili ili aendeleze miradi ya maendeleo inayofanywa na serikali yake

Rais wa Tanzania John Magufuli pamoja na makamu wa rais Samia Suluh
Rais wa Tanzania John Magufuli pamoja na makamu wa rais Samia SuluhuPicha: DW/S. Khamis

Akitumia zaidi ya dakika thelathini kuzungumza na wanachama wa CCM Rais Magufuli amesema, anawania kugombea kwa mara nyingine ili aweze kuendeleza miradi ya maendeleo iliokuwa ikitekelezwa na serikali yake, pamoja na kutekeleza ilani ya chama chake na kusisitiza kutafanyika kampeni za kistarabu na zinazozingatia sheria na taratibu za uchaguzi taifa ililojiwekea. 

Katibu mkuu wa chama hicho kilicho na wananchama zaidi ya milioni kumi na tano Bashiru Ally amesema CCM kimemchagua Magufuli kwa sababu amekuwa ni muadilifu na mnyenyekevu linapokuja swala la kuhudumia umma, kudhibiti ufisadi na rushwa kadhalika utekelezaji wa ilani hiyo, huku akisisitiza kazi ya kutafuta kura inakabidhiwa katika jumuia za chama hicho ikiwemo jumuia ya vijana, wazazi na wanawake wa chama hicho.Aliongeza

Mbali na chama cha mapinduzi ambacho kimechukua fomu tume ya taifa ya uchaguzi vyama vingine ambavyo vitachukua fomu ya urais ni pamoja na chama cha democrasia makini na Unaited Development People's Party UNDPP.

Mwandishi: Hawa Bihoga Dw Dar es salaam