1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Mpango mbadala wa May wa Brexit

Sekione Kitojo
31 Januari 2019

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na suala la mpango mbadala wa waziri mkuu Theresa May kuhusu kujitoa nchi yake katika Umoja wa Ulaya, changamoto zinazomkabili waziri wa ulinzi wa Ujerumani .

https://p.dw.com/p/3CUXt
Großbritannien Theresa May im Parlament Brexit Abstimmung
Picha: Reuters

Tukianza  na  mada  kuhusu  mpango mbadala  wa waziri  mkuu  wa Uingereza Theresa  May katika  Brexit, mhariri  wa  gazeti la  Rhein-Zeitung  anandika:

"Mbinu  za majadiliano  za Uingereza hazionekani kuwa na  mipango sahihi. Hali  hiyo imeonekana  kwa  muda  mrefu  sasa, na haijaondoka. Makampuni ya  kuunda  magari, tasinia ya  filamu, makampuni  ya  kutengeneza  madawa, hakuna  kinachokwenda, kwa kuwa  wanasubiri  kuidhinishwa  kwa  mpango  wa  Brexit  mwezi  wa Februari, na  inaonekana  kuwa  katika  kipindi  kijacho  hakutakuwa na suluhisho  kwa  kuwa  kuna  baadhi  ya  wanasiasa  nchini  humo ambao  wanamuonesha  waziri  mkuu  kuwa hafai  badala  ya kuangalia hali ya baadaye ya nchi  yao." 

Mhariri  wa  gazeti  la  Mannheimer anaandika  kuhusu  Brexit kwa kusema  kwamba  suala  la  hali  tete  ya  Ireland ya  kaskazini  kwa wanasiasa  wengi  lilionekana  kuwa si  kitisho. Mhariri  anaendelea:

"Hali  hiyo  inatia  wasi  wasi  na kushitua , ikiwa  ushahidi  lakini  pia ni  kwamba  serikali  ya  Uingereza  haitaki  kupata  kuaminika, kutokana  na  suala  hilo  la  eneo la  Ireland ya  kaskazini. Kwa  hiyo basi  Umoja  wa  Ulaya  unataka  kuhakikisha  maslahi  ya  watu  wa Ireland  yanalindwa. Suala  la  mpaka  halina  mjadala, na  pia  lisiwe suala  litakalotumiwa  kufanya  harakati  za  kisiasa  za chama  cha waziri  mkuu."

Waziri wa ulinzi

Kuhusiana  na  mada  juu  ya  jeshi  la  Ujerumani  kupata  vifaa muhimu  vya  kutendea  kazi, gazeti  la  Hannoversche Allgemeine Zeitung  linaandika:

"Waziri  wa  ulinzi  wa  Ujerumani  Ursula von der Leyen , alipoingia madarakani  alijaribu  kuweka  mambo  sawa  katika  wizara  hiyo, lakini  sasa  inaonekana  kwamba  hata  yeye  binafsi  yuko  gizani. Masuala  ya  kupanda  kupita  kiasi gharama za  meli  ya  mafunzo, ya Gorch Fock, na  mengineyo  katika jeshi  la  Ujerumani , na  washauri wa  nje  wa  wizara  kushindwa  kutoa  tahadhari  na  mapema  yanaonesha  wazi  kwamba  jaribio  la  Von der Leyen   kuweka kando  mara  kwa  mara  mpango  wa  kulipatia  vifaa  jeshi  ni  wazi kabisa  kwamba  mambo  mengi  hayaendi  sawa  na  si  rahisi  tena." 

Gazeti  la  Reutlinger General - Anzeiger  likizungumzia  kuhusu kuzuwia  shambulio  la  kigaidi  , linaandika:

"Kitisho  kwa  jamii  ya  Ujerumani  ni mipango  ile  ya  mashambulizi kuweza  kuzuwia  kwa  wakati  muafaka  kabla  ya  utekelezaji  wake, kwa  sababu  hali  hiyo  inachafua  utulivu wa  jamii  na  kusababisha watu  kutoa  hukumu  ya  kabla.  Hususan  kwa  wakimbizi , wanaonekana  kuwa  kuna  uwezekano  wa  wao  kufanya  shambulio la  kigaidi  kuliko  kwamba  hawa  ni  watu  wanohitaji  msaada  na kulindwa.  Hali  hii  inawapa fursa  wale  wenye msimamo  mkali  wa mrengo  wa  kulia ya kuonesha  chuki yao dhidi  ya  wageni. Kinachoshangaza  hiyo ndio  nadharia  ya  mafanikio  ya  kundi kama  la  IS, ili  kupambana  na  kile  inachokiita  mfumo  wa  mataifa ya  magharibi, wa kiliberali na mfumo unaotambua haja ya kuishi pamoja  licha ya  kutengana kimawazo."

 

Mwandishi: Sekione Kitojo / ilandspresse

Mhariri: Idd  Ismail Ssessanga