1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Kuanza kambi za kuwahifadhi wakimbizi Bavaria

Sekione Kitojo
2 Agosti 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi leo(02.08.2018) na taarifa ya kuanza kwa kambi za kuwahifadhi wakimbizi jimboni Bavaria, makundi ya uhalifu wa kupangilia nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/32Ujr
Pressekonferenz mit Horst Seehofer
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Horst SeehoferPicha: Reuters/F. Bensch

Mhariri  wa  gazeti  la Frankenpost  anaandika  kuhusu  kambi  za kuwahifadhi  wakimbizi: Mhariri  anaandika:

"Kambi  za  kuwahifadhi  wakimbizi  zimekwisha  andaliwa  kutokana na  mbinyo  wa  chama  cha  CSU, hii  ikiwa  ni  hofu  ya  wazi kutokana  na  uchaguzi wa  jimbo  la Bayern hapo Oktoba  14  bila kupoteza  wingi wake. Chama hicho  kinakabiliwa  na  hasira  ya umma kuhusu  mtazamo usiokubalika  dhidi  ya kile  kinachojulikana kama  wahamiaji  wa  kiuchumi. Chama  cha  CSU kimepitwa  na katika  uchunguzi wa  maoni  ya  wapiga  kura  na  kundi  la  wenye siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia, ambao  wanataka  kuchukuan hatua  kali  zaidi. Na  kwa  bahati  mbaya  wananchi  wanaunga mkono  msimamo  huo mkali. Na sasa  chama  cha  CSU kinataka kuchanganya masuala  ya  kidini  na  kijamii katika  suala  hili. Suala hilo halijapatiwa  suluhisho, watu  ambao  hawatapatiwa  haki  ya hifadhi  hapa  nchini  watalazimika  kurejeshwa  makwao. Mhariri anaandika  kwamba , makambi  ya  kuwahifadhi  wakimbizi yanahatari  ya  kugeuka  kuwa eneo  la  mabanda."

Mhariri  wa  gazeti  la  Rhein-Zeitung  la  mjini  Koblenz anazungumzia  pia kuhusu  kuanzishwa  kwa  makambi  ya kuwahifadhi  wakimbizi  jimboni  Bavaria. Mhariri  anaandika:

"Mawaziri  wakuu  wa  CDU  na  SPD walikutana , wakati  walipokuwa wakijadili  makubaliano  yao  ya  kuunda  serikali  ya  mseto. Kwa pamoja  walisema  kwamba  wazo  la  kuwa  na  makambi  ya kuwahifadhi  wakimbizi  si  jambo  zuri.  Imani  ya  waziri  wa  mambo ya  ndani  Horst Seehofer  kutoka  chama  cha  CSU  kwamba majimbo  mengine  huenda  yatafuata  nyayo  za  jimbo  lake  hazina msingi. Ni  jimbo  moja  tu  la  Saxony  lililokubaliana  na wazo  hilo. Chama  cha  CSU  hata  hivyo  kimejizuwia kufanya  sherehe kuhusiana  na  tukio  hilo  la  kufunguliwa  kwa  vituo  saba  vya kuwahifadhi  wakimbizi. lakini  pamoja  na  hayo  chama  hicho kimegundua  katika  kampeni  za   uchaguzi  kwamba  hatua  yao hiyo  haijawaletei tija."

Kuhusu  suala  la  uhalifu  wa  kupangilia, mhariri  wa  gazeti  la Wiesbadener kurier  anaandika  kwamba  Mwezi  Mei 1990 , karibu miaka  28  iliyopita , ulitolewa  ufafanuzi  kuhusu  kazi, kwa  mtazamo wa  polisi  na  mahakama  suala  la uhalifu  wa  kupangilia unawekwa wapi. Mhariri  anaadika:

"Je ufafanuzi  juu  ya  kazi unabeba mtazamo  sawa  kati  ya  kizazi kilichopita  cha  uhalifu  na  hii  leo ?  Nani  ana  haki  ya  kuuliza , iwapo  ufafanuzi  huo  wa  kazi  wa  wakati  huo  hauendani  na uhalifu  wa  wakati  huu , kuhusu  kitisho na  uwezo  wa  kuleta madhara  kupitia  makundi  yanayojitokeza , ambayo  sehemu  zao za  kazi zinaelezwa  kama  katika  mtandao  wa  internet. Ili kwa maslahi  ya  umma  iwezekane  kupambana  na  makundi  kama hayo!"

Naye  mhariri  wa  gazeti  la Frankfurter Allgemeine Zeitung akizungumzia  mada  hiyo  anaandika:

"Nchini  Ujerumani  hakuna  nafasi kwa makundi  ya  uhalifu  wa kupangilia, amesema  waziri  wa  mambo  ya  ndani Horst Seehofer. wakati  huo  huo mwanasiasa  huyo  kutoka  chama  cha  CSU anasema , makundi  ya  uhalifu  wa  kupangilia  yantishia  taifa  na uchumi  wa  nchi. Nini   maana  ya  kitisho  kwa  hiyo?  Mbinu  nyingi zimetumika  lakini  kila  wakati  kunaongezeka  uhalifu  wa kusafirisha  watu au  makundi  ya  kimafia.  Hakuna  sababu  ya msingi , katika umma  ulio katika  jamii  huru , ambapo  makundi  hayo ya  kihalifu  yanaweza  kufaidika, na  bila  shaka  yanapungua. Lakini pia  hakuna  sababu  ya  kubweteka na  kujaribu  kuyatetea  makundi kama  hayo  kupitia  mahakama ya  katiba."

Mhariri  wa  gazeti  la  Westfalenpost  anazungumzia  kuhusu  juhudi za  kampeni  inayojulikana  kama  Me Two  na  hali  ya  ubaguzi  ya kila  siku. Mhariri  anaandika:

"Ni  wakati  muafaka , sasa  wa  kubadilisha  mfumo  na  kuanza kusikiliza. Kwa  mfano , mtu  ambaye  anakabiliwa  na  ubaguzi  hata mdogo  tu  na  haaminiki, kwamba  amekabiliwa  na  hali  hiyo.  Hii  ni pamoja  na  ukosoaji  kuhusu  kuishi  pamoja, ni  vizuri  kuliangalia upya  suala  hilo. Kwamba  iwapo  mtu  anapenda  kula  nyama  ya nguruwe  ama  hapendi, si  suala  la  kujadiliwa  hapa, kwamba  yeye ni Mjerumani  safi. Katiba  haina uhusiano na  suala  hilo. Sheria inakwenda  kwa  kila  mtu, ambae anataka  kuishi  katika  nchi  yetu. Tunapaswa  kuliangalia  vizuri  suala  hilo."

Hayo ndio  maoni  ya  wahariri  wa  magazeti  ya  Ujerumani hii  leo kama  yalivyokusanywa  na  Sekione  Kitojo.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Josephat  Charo.