1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Boris Johnson madarakani mtaa wa Downing

Sekione Kitojo
24 Julai 2019

Wahariri wa magazeti  karibu  yote ya  Ujerumani wameandika kuhusu mabadiliko ya utawala  nchini  Uingereza  ambapo Boris Johnson  ameingia  sasa  madarakani akiwa  waziri  mkuu.

https://p.dw.com/p/3MeYM
Großbritannien London | Boris Johnson posiert vor dem Hauptquartiert der Konservativen
Picha: Getty Images/D. Kitwood

 

Tukianza  na  gazeti  la  Frankfurter Allgemeine Zeitung , mhariri anaandika  kwamba  itakuwaje  pale  mtu  huyu mtu  katika  ofisi  ya waziri  mkuu  ya  mtaa  wa  Downing  namba 10  atakavyokuwa mara akitambua  ugumu  wa majukumu yake, hususan  atakapoanza kuona  uzito wa  uwajibikaji. Mhariri  anaandika:

"Mzozo wa  Uingereza  na  Iran, unaonesha  kile  kitakachotokea  kwa Boris Johnson. Umoja  wa  Ulaya  unaonesha  uvumilivu dhidi ya uchokozi unaofanyiwa  mwanachama  wake, dunia  lakini  haisubiri, hadi  pale  wanasiasa  wa  Uingereza watakapouzima. Ni kwa  kiasi gani  uhusiano  katika  ya  Uingereza  na  Ulaya  utakuwa  wa karibu, na  ni  ukaribu  wa  kiasi  gani  mwanasiasa  huyu Johnson atajongeleana  na  rais  wa  Marekani. Trump  amempaka  mafuta mara  kadhaa, na  kwa  hiyo  Johnson  hapaswi  kulewa  na  sifa hizo. Kwa  upande wao mataifa  ya  Ulaya  yanamuhitaji , kadiri ya inavyowezekana, kumnyooshea  mkono, lakini  si  bila  shaka kutafuta  kuitumbukiza  Uingereza  shimoni."

Nae mhariri  wa  gazeti  la  Stuttgarter Zeitung  akindika  kuhusu kuingia  madarakani  kwa  Boris Johnson  anasema:

Großbritannien London | Boris Johnson wird neuer Premierminister
Waziri mkuu mpya wa Uingereza Boris JohnsonPicha: Reuters/T. Melville

"Johnson anakalia  kuti  kavu  katika  madaraka  yake. Wingi  katika bunge  ni  mwembamba  mno, anaweza  wakati  wowote  kupigiwa kura  ya  kutokuwa  na  imani  nae  bungeni. Na   wengi  wa wabunge  wanapinga  makubaliano ya  kujitoa  kutoka  Umoja  wa Ulaya  Brexit bila  ya  kupata  makubaliano.  haujaondoka uwezekano , kwamba  badala  ya  Brexit  kunaweza  kuwa na uchaguzi  mpya  nchini  Uingereza  na kura  ya  pili  ya  maoni ifikapo mwishoni  mwa  mwaka  huu kutokana  na  matokeo  ya kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya."

Mhariri  wa  gazeti  la  Leipziger Volkszeitung , nae  anaandika kuhusu  kuingia  madarakani  kwa  Boris Johnson  nchini  Uingereza. Mhariri  anasema:

"Katika  siku  ya  kwanza  tu  katika ofisi  ya  mtaa  wa  Downing Johnson atatambua, kwamba  sio  tu Brexit , badala  yake  suala  la Iran  ndio  mada  muhimu  zaidi  inayomsubiri. Katika  mzozo  na Iran wanadiplomasia  wa  Uingereza, wanataka  haraka  kuweka umoja katika  Umoja  wa  Ulaya  kuunda ujumbe wa kikosi cha kulinda mlango  bahari  wa  Hormuz. London inataka  kwa  hiyo , kuwa karibu na  Umoja  wa  Ulaya. Mhariri  hata  hivyo  anauliza  , ni  vipi inawezekana  kwenda  pamoja  na  wanasiasa  wa  Uingereza , wakati  lengo  la  wanasiasa  hao  ni  kujitoa  kutoka  Umoja  wa Ulaya."