1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafunzo ya densi mtindo wa ‘Ballet’ Lagos Nigeria

26 Oktoba 2020

Hii ni shule ya densi mtindo wa Ballet katika mtaa wa watu maskini kwenye mji mkubwa Lagos nchini Nigeria. Hutoa mafunzo ya densi maalum kwa watoto katika taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu Afrika. Daniel Ajala anayependa densi ya ballet, aliifungua shule hii mwishoni mwa mwaka 2017 baada ya kusomea mbinu za densi hiyo vitabuni na mitandaoni.

https://p.dw.com/p/3kR1E