1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Maelfu ya raia wa Kongo waomba hifadhi Burundi

17 Februari 2025

Raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wapatao elfu 10 wamevuka mpaka na kuingia kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini Burundi, serikali ya Bunjumbura aimesema kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa inachukua hatua muhimu.

https://p.dw.com/p/4qbl9
DR Kongo 2025 | Raia wa Kongo wanaosaka hifadhi
Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa njiani kusaka hifadhi maeneo salamaPicha: TONY KARUMBA/AFP

Waziri wa mambo ya ndani na usalama wa Burundi amesema Serikali ya nchi hiyo kwa ushirikiano na Shirika la Wakimbizi, UNHCR zimo katika zoezi la kukagua wenye kutimiza vigezo vya kuwa wakimbizi.

Wakati huo huo mwakilishi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP na Afisa anaye husika na usalama kwenye shirika hilo wamefukuzwa kutoka Burundi. Wanatuhumiwa kuwataka wafanyakazi wa WFP kuwa makini kwenye kanuni za tahadhari za kiiusalama. 

Katika mahojiano na waandishi bahari baada ya kuzuru maeneo ya mpaka kati ya Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, waziri wa mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama, amesema raia wa Kongo elfu 10 wamekwisha ingia Burundi kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Soma pia:Serikali ya Kongo yathibitisha kuwa M23 imechukua udhibiti wa mji wa Bukavu

Waziri Martin Niteretse amesema kuwa, kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa mataifa la huduma kwa wakimbizi UNHCR, wamekuwa katika zoezi la kukagua wenye kutimiza vigezo ili waweze kukubaliwa kuwa wakimbizi.

"Kila mmoja anatakiwa kutambulika, hivyo raia hao kutoka DRC, waweze kutenganishwa wanajeshi na raia wa kawaida, wagonjwa, aidha wenye kuhitaji huduma za haraka, wanawake waja wazito,na watoto"

Oparesheni ya kuwakamata wanaoishi kinyemela

Kuhusiana na kamata kamata raia wa kigeni iliyo fanyika mnamo siku za nyuma nchini, Waziri Niteretse amesema ni operesheni ya kawaida ya polisi ya taifa, na kwamba watu wapatao 80 wamekwisha kamatwa baada ya kukutwa hawana vitambulisho huku wengine wakiwa na vitambulisho visivyo halali.

Nani ananufaika na machafuko ya Kongo?

Waziri huyo wa Mambo ya Ndani maendeleo ya jamii na usalama wa taifa, amewatuliza nyoyo raia, kwa kuwaambia kwamba vita vinavyo endelea mashariki mwa Kongo haviwezi kuhatarisha usalama wa Burundi.

 Hali inayojiri Kongo, haiwezi kuhatarisha usalama wa Burundi. Warundi watakiwa kusalia tulivu, Rais wa jamuhuri aliwambia kuwa, wamezungumza na wenzi wao wa Rwanda, na kuwahakikishia kuwa hakuna kitakacho haribika."

Soma pia:Vyanzo: Waasi wa M23 wameingia mji wa Bukavu

Hayo yanajiri wakati mwakilishi wa mpango wa chakula duniani WFP, Sidibi Lawson Mariot na Sarah Nguen mkuu wa kitengo cha usalama kwenye shirika hilo, wamefukuzwa nchini baada ya kupewa muda wa saa 48 kuwa wameondoka.

Maafisa hao wawili WFP wanatuhumiwa kutoa taarifa zinazohatarisha hali ya usalama nchini, baada ya kuwataka wafanyakazi wa shirika hilo kuwa makini juu ya za tahadhari zakiiusalama.

Tayari maafisa hao wameondoka Burundi na kuelekea katika nchi jirani ya Rwanda.