1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maduro aufungia mtandao wa X

9 Agosti 2024

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesaini azimio la kuufungia mtandao wa kijamii wa X kwa siku 10 wakiutuhumu kuchochea machafuko baada ya uchaguzi wa mwishioni mwa mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4jHey
Venezuela Caracas | Nach Präsidentenwahl | Präsident Nicolas Maduro
Picha: Jeampier Arguinzones/dpa/picture alliance

Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo wa tarehe 28 Julai, ambao Maduro ametangazwa mshindi, Maduro amekuwa akijibizana vikali na mmiliki wa mtandao wa X, Elon Musk, ambaye naye amekuwa akituma taarifa za kumpiga Maduro.

Hayo yakijiri, kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado, amesema anahofia kutakuwa na ongezeko kubwa la Wavenezuela wanaoikimbia nchi yao, endapo Maduro ataendelea kusalia madarakani.

Akizungumza na waandishgi wa habari kwa njia ya vidio hapo jana, Machado alisema anakisia raia wapatao milioni tatu hadi tano watahama nchi yao kwa wakati mmoja.

Upinzani unadai kuwa mgombea wao, Edmundo Gonzalez, ndiye aliyeshinda uchaguzi huo, na wametowa wito wa kuwekwa hadharani kwa matokeo halisi ya uchaguzi huo.