1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron:Uhuru ndani ya Morocco ni suluhu kwa Sahara Magharibi

Josephat Charo
30 Julai 2024

Ufaransa leo imesema uhuru ndani ya Morocco ndiyo msingi pekee wa suluhisho la mzozo uliodumu miongo kadhaa wa eneo la Sahara Magharibi.

https://p.dw.com/p/4iuvo
Berlin, Ujerumani - Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Kansela.
Berlin, Ujerumani - Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Kansela.Picha: Ruffer/Caro/picture alliance

Kauli hiyo imeibua ukosoaji wa ghadhabu kutoka kwa Vuguvugu linalopigania uhuru wa Sahara Magharibi la Polisario Front. Katika barua kwa Mfalme Mohammed VI ya kumpongeza wakati wa maadhimisho ya miaka 25 tangu alipotawazwa kuwa mfalme, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema pendekezo la Morocco sasa ndilo msingi pekee utakaopelekea kupatikana kwa suluhisho la kisiasa la haki na la kudumu litakaloendana na maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kasri la Mfalme wa Morocco limeyapongeza matamshi ya Macron katika barua yake kama hatua muhimu ya kuunga mkono uhuru wa Morocco dhidi ya Sahara Magharibi. Chama cha Polisario kimejibu kikisema Macron anaunga mkono hatua ya matumizi ya nguvu na ya kinyume na sheria yanayofanywa na Morocco.