1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron aelezea wasiwasi juu ya hatima ya Bazoum

21 Oktoba 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea wasiwasi wake juu ya hali ya sintofahamu inayomkabili rais aliyeondolewa madarakani wa Niger Mohamed Bazoum.

https://p.dw.com/p/4Xq7L
Nigeria | Welt-Blutspende-Tag
Picha: Niger Prasidential Website

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea wasiwasi wake juu ya hali ya sintofahamu inayomkabili rais aliyeondolewa madarakani wa Niger Mohamed Bazoum. Kauli ya Macron inafuatia taarifa iliyotolewa na watawala wa kijeshi kwamba Bazoum alijaribu kutoroka. Macron ametoa wito wa kumwachilia mara moja rais huyo na familia yake.

Tangu alipopinduliwa na jeshi mnamo Julai 26, Bazoum amekuwa akizuiliwa katika makazi yake pamoja na mkewe na mwanawe wa kiume. Mawakili wa Bazoum wameyakataa madai hayo huku mratibu wa kundi la wanasheria Mohamed Seydou Diagne, akisema katika taarifa kuwa wanapinga vikali shutuma hizo za uzushi dhidi ya rais Bazoum na kusisitiza kwamba utawala wa kijeshi umevuka mstari mwekundu kwa kumshikilia rais huyo sehemu kusikojulikana na kwamba hilo linakiuka haki zake za msingi.