1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Macron aitisha mkutano mwingine kuhusu New Caledonia

Sylvia Mwehozi
20 Mei 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitisha mkutano mwingine wa dharura wa baraza lake la ulinzi na usalama leo kwa ajili ya kujadili ghasia zinazoendelea katika kisiwa cha New Caledonia ambacho ni himaya yake.

https://p.dw.com/p/4g3hZ
New Caledonia-ghasia
Maafisa wa usalama wakiondoa vizuizi barabaraniPicha: Delphine Mayeur/AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitisha mkutano mwingine wa dharura wa baraza lake la ulinzi na usalama leo kwa ajili ya kujadili ghasia zinazoendelea katika kisiwa cha New Caledonia ambacho ni himaya yake. Huu ni mkutano wa tatu kuitishwa na Macron chini ya wiki moja. Mikutano ya awali ilitoka na maamuzi ya kutangaza hali ya hatari na kutuma wanajeshi ili kusaidia vikosi vya serikali ya kisiwa hicho kurejesha utulivu.

Kwanini New Caledonia imekumbwa na ghasia?

Hapo jana, wanajeshi wa Ufaransa walikuwa na kazi ya kuondoa vizuizi katika barabara kuu inayoelekea uwanja wa ndege. Mnamo siku ya Ijumaa waziri mkuu wa Ufaransa Gabriel Attal alikutana na viongozi wa vyama vya siasa bungeni kujadili mgogoro huo na haswa suala la kurefusha hali ya hatari baada ya siku 12 za awali.