1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabishano yanaendelea kama Zanzibar ni nchi?

Miraji Othman18 Julai 2008

Mkuu wa upinzani Zanzibar anasema Zanzibar ni nchi.

https://p.dw.com/p/EeuE
Mji mkongwe wa ZanzibarPicha: DW /Maya Dreyer

Bado mabishano yanaendelea huko Tanzania kama Visiwa vya Zanzibar ni nchi ama sivyo. Spika wa Baraza la wawakilishi huko Zanzibar amezuwia kusikilizwa hoja ya kiongozi wa upinzani wa Chama cha CUF, Aboubakar Khamis Bakari, kutaka suala hilo lijadiliwe barazani. Spika anahoji kwamba suala hilo linajadiliwa baina ya wanasheria wa serekali za Muungano na ile ya Zazibar. Itakumbukwa kwamba chimbuko la mabishano haya lilianza pale waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, aliposema bungeni kwamba Zanzibar sio nchi. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Salma Said, amefanya mahojiano na Aboubakar Khamis Bakari, na alikuwa na haya ya kusema kuhusu hoja aliotaka kuiwasilisha...