1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabadiliko zaidi ndani ya CCM Tanzania

15 Machi 2017

Chama tawala nchini Tanzania, CCM kimepanga kufanya mabadiliko zaidi katika kile wanachosema kukiboresha chama nchi katika uongozi wake wa awamu ya tano.

https://p.dw.com/p/2ZCBG

Baada ya kumalizika mkutano mkuu maalumu wa chama tawala nchini Tanzania  chama cha  mapinduzi CCM uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni  chama hicho kimeazimia kufanya mabadiliko mengine makubwa ndani ya chama hicho yenye lengo la kukiimarisha na kuongeza tija. Isaac Gamba amezungumza na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole kutaka ufafanuzi zaidi kuhusina na mabadiliko hayo.