1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandalizi ya kandanda kurudi England yapamba moto

18 Mei 2020

Baadhi ya vilabu huko England vimeanza kuwapima wachezaji wao virusi vya corona kwa ajili ya kujiweka tayari kurejelea mechi za ligi hiyo.

https://p.dw.com/p/3cQYL
Fußball FC Liverpool Trent Alexander Arnold Einwurf
Picha: AFP/O. Scarff

Mechi hizo pia zitachezwa bila mashabiki uwanjani, iwapo hakutokuwepo na ongezeko la maambukizi kufikia mwanzoni mwa mwezi ujao wa Juni.

Nchini Uhispania nako kandanda liko karibu kurejea baada ya mapumziko marefu kutokana na janga la virusi vya corona. Rais wa Ligi Kuu ya Uhispania Javier Tebas amethibitisha kwamba kuanzia leo timu zimekubwaliwa kuanza kufanya mazoezi kwa makundi ya wachezaji kumi kumi. Tebas alionya kwamba endapo msimu hautokamilishwa basi huenda vilabu vikapoteza hadi yuro bilioni moja.

Wiki iliyopita, wachezaji walianza kufanya mazoezi katika vilabu vyao ingawa kila mmoja alikuwa akifanya mazoezi kivyake.