1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Ujumbe wa Marekani wakutana na wawakilishi wa Taliban, Doha

1 Agosti 2023

Maafisa wa Marekani walikutana na wawakilishi wa Taliban mjini Doha, ambapo walishutumu kudhoofika kwa hali ya haki za binaadamu nchini Afghanistan hasa za wanawake na wasichana.

https://p.dw.com/p/4Uccz
Maafisa wa Marekani wakutana na wawakilishi wa Taliban mjini Doha, Oktoba 12, 2021
Maafisa wa Marekani wakutana na wawakilishi wa Taliban mjini DohaPicha: Stringer/REUTERS

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imesema ujumbe wa Marekani katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Qatar Jumapili, ulielezea wasiwasi mkubwa kuhusiana na mzozo wa kiutu na haja ya kuendelea kuyaunga mkono mashirika ya misaada na taasisi za Umoja wa Mataifa zinazotoa msaada kwa kuzingatia kanuni za kibinaadamu nchini Afghanstan.

Ujumbe wa Marekani waelezea wasiwasi kuhusu unyanyasaji

Aidha walionyesha wasiwasi mkubwa kuhusu matukio ya kukamatwa watu, ukandamizaji wa vyombo vya habari, na mipaka kuhusu masuala ya kidini.

Waliohudhiuria ni pamoja na Mwakilishi Maalum wa Marekani Thomas West na Mjumbe Maalum anayehusika na Wanawake wa Afghanistan, Wasichana na Haki za Binaadamu Rina Amiri, pamoja na Karen Decker, mkuu wa ujumbe wa Marekani nchini Afghanistan. Taarifa hiyo haikutoa maelezo ya wawakilishi wa Taliban walioshiriki mazungumzo hayo