M23 wakaribia kuudhibiti mji muhimu mashariki mwa DRC
4 Januari 2025Waasi wa M23 wamesogea karibu na mji muhimu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Ijumaa na kuliteka eneo la karibu.Mazungumzo ya amani kati ya DRC na Rwanda yafutwa
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyozungumza na shirika la habari la AFP, waasi wa M23 walikuwa wamechukua udhibiti wa eneo la Katale, mahali pa mwisho ambapo waasi wanapaswa kupita kabla ya kuingia Masisi, mji mkuu wa kiutawala wa eneo la Masisi.
Rais wa asasi za kiraia za Masisi, Telesphore Mitondeke akizungumza na AFP alithibitisha vifo kadhaa vya raia vilivyotokea wakati wa mapigano katika eneo hilo.
Waasi wa M23wanaodaiwa kuungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda na jeshi lake, wameteka maeneo makubwa ya mashariki mwa DRC tangu mwaka 2021, na kusababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao na mgogoro wa kibinadamu.