1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lyon, Ufaransa. Moto wazuka katika barabara ya chini ya ardhi katika milima ya Alps barani Ulaya na kusababisha vifo vya madereva wawili.

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6u

Kumezuka moto mwingine katika barabara ya chini ya ardhi katika milima ya Alps barani Ulaya, miaka sita baada ya maafa yaliyotokea huko Mont Blanc. Usiku wa jana , lori lililokuwa limebeba matairi lilishika moto katika barabara hiyo ya chini ya ardhi ya Frejus, kati ya Lyon nchini Ufaransa na Turin nchini Itali na kusababisha vifo vya madereva wawili wa malori kutoka Slovenia.

Moto huo ulianza katikati ya barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 13 chini ya ardhi.

Shirika la habari la Italia ANSA limesema kuwa kiasi cha madereva 20 waliathirika kwa moshi waliouvuta na wameokolewa na wazima moto. Magari yamezuiwa kupita katika njia hiyo . Moto huo umezuka licha ya hatua za kiusalama zinazochukuliwa katika barabara hiyo tangu kuzuka kwa maafa ya Mont Blanc mwaka 1999 ambapo watu 39 walikufa.