1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA:Mtuhumiwa wa ugaidi anayezuiliwa Zambia kukabidhiwa kwa Uingereza

31 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEp9

Zambia inajiandaa kumkabidhi raia wa Uingereza mwenye asili ya Kihindi aliyekamatwa siku kumi na moja zilizopita kwa Uingereza.

Serikali ya Zambia imethibitisha kumzuilia ndani Haroon Aswat aliyekamatwa Julai 20 mjini Lusaka.

Marekani pia imeomba kukabidhiwa mtuhumiwa huyo wa kupanga mashambulio ya mabomu ya julai 7 mjini London, lakini baada ya majadiliano ya muda miongoni mwa maafisa wa zambia imeamuliwa mtuhumiwa huyo kukabidhiwa Uingereza.

Kwa mujibu wa Afisa mmoja wa Zambia Aswat huenda akakabidhiwa kwa Uingereza jioni hii.

Hata hivyo shirika la ujasusi la Uingereza Scotland Yard halijathibitisha iwapo Aswat ni mshukiwa wa ugaidi huku likizitaja ripoti za vyombo vya habari kuwa dhana.