1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Zambia yaukataa mswada wa katiba mpya

3 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEMJ

Serikali ya Zambia imeukataa mswada wa katiba mpya ya nchi hiyo uliotayarishwa na tume maalumu iliyoundwa na serikali, baada ya maandamano kufanyika katika sehemu mbalimbali nchini humo.

Waziri wa sheria wa Zambia, George Kunda, amesema katika taarifa yake kwamba serikali inauchunguza upya mswada huo kuhakikisha unaendana na hali ya taifa hilo na kuweza kukubalika na wengi huku uchaguzi ukikaribia kufanyika mwaka ujao.

Lakini wanasiasa wa upinzani na wanachama wa makundi mbalimbali ya kijamii wameusifu mswada huo wakisema unawapa raia haki zaidi na kupunguza mamlaka makubwa ya rais.