1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Zambia yamrejesha nyumbani mtuhiwa wa kigaidi

8 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmx

Zambia imemrejesha nyumbani mtuhumiwa wa kigaidi raia wa Uingereza, Haroon Rashid Aswad. Polisi ya Uingereza imesema atakapowasili nchini humo, Aswad huenda akahamishwa hadi Marekani ambako anatafutwa kwa tuhuma za kuhusika katika juhudi za kuanzisha kambi ya mafunzo ya wanamgambo katika jimbo la Oregon.

Aswad alitiwa mbaroni tarehe 20 mwezi uliopita kwa tuhuma za kuhusika katika mashambulio ya mabomu ya Julai saba mjini London, Uingereza, lakini polisi wanafikiri hakuhusika katika mashambulio hayo.