1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA : Zambia yafunga mpaka na Tanzania

1 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDGE

Zambia imeufunga kwa muda mpaka wake na Tanzania kufuatia ghasia za hapo jana usiku ambazo zimepelekea kujeruhiwa kwa watu kadhaa na kuharibiwa kwa mali.

Mkuu wa wilaya ya kaskazini mwa Zambia Edwin Sinyinza amesema ghasia hizo zimezuka jana usiku baada ya kupatikana habari kwamba raia mmoja wa Tanzania amekufa akiwa kizuizini mwa polisi katika mji wa mpakani wa Zambia wa Nakonde.

Amesema wameufunga mpaka huo kuwezesha kurudi kwa hali ya utulivu.

Ameongeza kusema kwamba baadhi ya magari na nyumba zilitiwa moto wakati Wazambia waliokuweko upande wa mpaka wa Tanzania walijeruhiwa vibaya na watu waliokuwa wakifanya fujo kabla ya polisi kutoka pande zote mbili kuingilia kati na kutuliza ghasia hizo.