1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lukashenko asema nchi za Magharipi zinapanga kumhujumu

26 Mei 2021

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amezituhumu nchi za Magharibi kujaribu kutumia tukio la kulazimishwa kutua mjini Minsk ndege ya Ryanair mwishoni mwa wiki ili kuanzisha vita vya kisiasa dhidi yake

https://p.dw.com/p/3tyar
Belarus Minsk | Rede Alexander Lukashenko im parlament
Picha: Maxim Guchek/BelTA/REUTERS

Lukashenko amesema nchi hizo zimesema uwongo kueleza jinsi alivyolishughulikia tukio hilo. 

Katika matamshi yake ya kwanza baada ya baadhi ya wanasiasa wa Ulaya kuliita tukio hilo la Jumapili kuwa ni "utekaji nyara uliofadhiliwa na serikali", Lukashenko ameliambia bunge kuwa alichukua hatua halali na kwa mujibu wa sheria zote za kimataifa, lakini watu wenye nia mbaya wanajaribu kutumia tukio hilo la ndege kuhujumu utawala wake.

soma zaidi: Viongozi walaani kukamatwa mwanaharakati wa Belarus

Belarus ilitumia kisa hicho kumkamata mwandishi wa habari wa siasa za upinzani aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo Raman Pratasevich.

Kiongozi wa upinzani aliyeko uhamishoni Sviatlana Tsikhanouvskaya amesema leo kuwa upinzani unajiandaa kwa awamu mpya ya maandamano ya kuipinga serikali nchini Belarus.