1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Luiz Inacio Lila Da Silva kuitumia EU pendekezo la MERCOSOR

19 Julai 2023

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lila Da Silva amesema atatuma pendekezo mbadala kwa Umoja wa Ulaya kuhusu muafaka wa biashara uliocheleweshwa na jumuiya ya nchi za Amerika Kusini katika wiki mbili au tatu zijazo.

https://p.dw.com/p/4U79O
Rais wa Brazili akiwa katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na rais wa Venezuela ambaye hayuko pichani huko Brasilia nchini Brazili mnamo Mei 29 2023
Rasi wa Brazil Lula da SilvaPicha: Frederico Brasil/TheNews2/IMAGO Images

Lula, aliyezungumza baada ya mkutano wa kilele wa siku mbili kati ya Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Mataifa ya Amerika Kusini na Caribbean mjini Brussels, amesema Brazil imetayarisha jibu ambalo sasa linajadiliwa na nchi za Soko la Pamoja la Amerika Kusini, ambalo pia linazijumuisha Argentina, Paraguay na Uruguay.

Lula anaamini pendekezo hilo litakubaliwa na Umoja wa Ulaya

Rais huyo wa Brazil amesema anaamini kuwa Umoja wa Ulaya utalikubali kwa urahisi sana. Umoja wa Ulaya na jumuiya hiyo zilikamilisha mazungumzo mwaka wa 2019 lakini mpango huo umesimama kwa muda kutokana na wasiwasi kuhusu ukataji miti katika msitu wa Amazon na dhamira ya Brazil kuhusu hatua za kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Lula, aliyechaguliwa mwaka jana, ameahidi kuifanyia mabadiliko sera ya nchi yake ya mazingira.