1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUANDA. Watu 210 wafariki dunia Angola kkwa sababu ya virusi wa Marburg.

13 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNd

Shirika la afya duniani, WHO, limetangaza kwamba watu 210 wamefariki dunia nchini Angola kufuatia maradhi yanayosababishwa na virusi wa Marburg. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na shirika hilo na wizara ya afya nchini humo, inasema watu wengine 361 wanaangaliwa na madaktari katika maeneo mbalimbali chini humo. Virusi hao wana uwezo wa kumuua mtu katika kipindi cha juma moja, na kufikia sasa hakuna tiba ya maradhi hayo. Maradhi mabaya zaidi yalizuka katika jamhuri ya kidemokrsi ya Congo, ambako watu 123 walifariki dunia kati ya mwaka wa 1998 na 2000.